×

Azam Wana Mzuka Kinoma Kuwavaa Mbeya City

Wachezaji wa Azam FC

KUELEKEA mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa leo Jumamosi, Azam FC imesema ina hamu kubwa ya kupata ushindi ili kuweka heshima katika Ligi Kuu Bara baada ya kutolewa katika Kombe la FA.

 

Azam wanaonolewa na Kocha Aristica Cioaba raia wa Romania, leo watakuwa wageni wa Mbeya City walio chini ya Kocha Ramadhan Nswanzurimo kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

Mromania huyo ameliambia Championi Jumamosi, kwamba wao wako vizuri kwa ajili ya mechi hiyo ambapo lengo lao ni kupata pointi tatu kwa ajili ya kujitengenezea heshima ikiwezekana hata kutwaa ubingwa endapo Simba na Yanga zitateleza.

STORI: SAID ALLY