×

HATIMAYE MWILI WA LEYLA WAWASILI TANZANIA, KUZIKWA ARUSHA

Taswira ya nyumbani kwao marehemu, leo Aprili 23, 2018.

 

Mwili wa Mtanzania, Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na mumewe, Kema Kasambula, mwezi uliopita jijini London nvhini Uingereza  umewasili nchini leo  Jumatatu, Aprili 23, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupelekwa nyumbani kwao. Arusha kwa ajili ya shughuli ya mazishi.

 

Leyla enzi za uhai wake akiwa na mumewe.

 

Mwili wa Leyla ulikuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia.

 

Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo ambapo sasa jamaa huyo anakabiliwa na kesi ya mauaji.

 

Leyla ni mtoto wa Hidaya aliyeimbwa na Pepe Kalle kwenye wimbo wake wa Hidaya miaka ya 1990, mwenye makazi yake Kaloleni jijini Arusha ambako ndiko msiba ulipo. Taratibu za mazishi ya Leyla zitaanza kufanyika kesho Jumanne nyumbani kwao Arusha.

 

PICHA NA COLUMBA MOSHI | GLOBAL TV, ARUSHA

UTALIA! Mwili wa Masogange Ulivyowasili Kwao, Vilio Vyatawala!