MSANII wa Bongo Fleva, Janabi Mmbaraka (Jebby) maarufu kama Swahiba, aliyefariki dunia jana mchana, amepumzishwa katika nyumba yake ya milele mjini Dodoma leo Jumanne, Aprili 23, 2018.

Jebby amefariki dunia jana Jumapili, Aprili 22, 2018 nyumbani kwao huko Dodoma ambapo taarifa zinasema alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye bandama na upungufu wa damu.

Jebby atakumbukwa kwa wimbo wake wa ‘Swahiba’ aliomshirikisha Afande Sele. Wiki iliyopita Jebby aliomba kurudishwa kwao Dodoma baada ya hali yake kubadilika.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.