Simba, Shiza Kichuya juzi Jumamosi aliwashangaza wengi baada ya kuamua kucheza na fedha ambazo alipewa na mashabiki wa timu hiyo.
Kichuya alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kilikuwa ugenini kuvaana na Singida United katika pambano la Ligi Kuu Bara lililopigwa katika Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Katika mchezo huo Kichuya mwenye mabao saba katika ligi hakufanikiwa kuanza katika kikosi cha kwanza, hivyo kuanzia benchi akiwa na nyota wengine kadhaa.
Championi Jumatatu ambalo lilikuwepo uwanjani hapo lilimshuhudia Kichuya akimwagiwa fedha na mashabiki mbalimbali wa timu hiyo kiasi kinachofikia shilingi laki mbili (200,000) ambao walimpa fedha hizo wakati nyota huyo akiwa benchini.
Kutokana na kutokuwa na sehemu ya kuzihifadhi fedha hizo, Kichuya alizikunja fedha hizo na kuzitia katika soksi zake na kuingia uwanjani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.
Simba walishinda mchezo huo kwa bao 1-0 na kuifanya kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa kwa msimu huu hadi sasa. Bao lao lilifungwa na Shomary Kapombe.
Musa Mateja, aliyekua Singida.