
RAIS John Magufuli amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali na Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa.
Kabla ya uteuzi huo Jaji Wambali alikuwa Jaji Kiongozi na Jaji Kwariko alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Uteuzi huu umeanza jana Juni Mosi, 2018.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema tarehe ya kuapishwa kwa majaji hao itatangazwa hapo baadaye.
Pia, Rais amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini mbapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Madini na alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua David Mulabwa kuwa Kamishna wa Madini.

Aidha, Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa nne wa Jeshi la Magereza kutoka Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP) na kuwa Kamishna wa Magereza (Commissioner of Prisons – CP) na kuwapandisha vyeo maofisa wengine watano katika jeshi hilo kutoka Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (Senior Assistant Commissioner of Prisons – SACP) kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (Deputy Commissioner of Prisons – DCP).
Maofisa hao waliopandishwa vyeo kutoka DCP na kuwa CP ni kama ifuatavyo;
1. Hamis Ngarama
2. Tusekile Mwaisabila
3. Augustine Sangalali Mboje
4. Gideon Marco Nkana
