
Muasisi wa Kampuni ya TICTS ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera, Nazir Karamagi amesema anaunga mkono uwekezaji mpya katika Bandari ya Dar es Salaam, hasa baada ya Kampuni yake Kumaliza mkataba wa Kuhudumia Bandari hiyo, ambayo ni muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.
Karamagi ametoa Kauli hiyo Leo Julai 30, 2023 Jijini Mwanza mbele ya Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo wakati wa Mkutano wa Hadhara Uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.