
Jina la Dalai Lama limekuwa gumzo duniani kote baada ya mtu huyo kukumbwa na kashfa nzito ya kulazimisha mtoto ambusu mdomoni na kumnyonya ulimi!
Mtu huyo Dunia inamfahamu kama Dalai Lama wa 14; kiongozi mkuu wa nchi iitwayo Tibet ambayo inapatikana katika Milima ya Himalaya huko barani Asia.
Pia Dalai Lama ni kiongozi kiroho wa imani ya Kibuddha kama ilivyo Baba Mtakatifu (Papa) kwa Wakristo au Ayatollah Khomeini kwa Waislam. Dalai Lama pia ni mtaalam wa masuala ya vifaa vya umeme (electronics). Dalai Lama anazungumzwa mno kwa sasa baada ya Jumatatu iliyopita kulazimika kuomba radhi kwa kitendo chake cha kumlazimisha mvulana mdogo amnyonye ulimi wake wiki chache zilizopita ambapo video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia kali.