×

Msalaba wa Banana na Gumzo kwa Mashabiki

Banana Zorro

MKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva, Banana Zorro amezua gumzo usiku mnene ukumbini baada ya kuonekana akiwa ametinga msalaba shingoni wenye sanamu ya Yesu Kristo msalabani huku ikifahamika kuwa ni Muislam.

Tukio hilo lililoacha midomo wazi mashabiki wengi waliojitokeza, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Legend Park, Namanga jijini Dar ambapo Banana hufanya shoo na bendi yake ya B-Band.

Ishu ilianza kama utani kwa baadhi ya mashabiki kuanza ‘kuudiskasi’ msalaba huo wa silva uliokuwa pamoja na cheni yake huku wengi wakihoji uhalali wa dini yake na kitu alichovaa.

“Vitu vingine ni kuviacha kama vilivyo, hebu ona anavaa mambo ya dini hadi ukumbini, bora basi angekuwa Mkristu yule ni Muislam safi,” alisema shabiki mmoja.

Star Showbiz baada ya kuwasikia mashabiki hao, lilimsubiri Banana ashuke jukwaani liweze kumuuliza ambapo aliposhuka tu lilimuwahi na kumhoji.

Star Showbiz: Hongera kwa makamuzi na bendi yako!

Banana: Asante sana.

Star Showbiz: Kwa muda mrefu umedumu kwenye gemu nini siri yake?

Banana: Mazoezi na kutokukata tamaa bro!

Star Showbiz: Nakuona na msalaba shingoni wenye imani ya dini ya Kikristo, tunajua wewe ni Muislam hii imekaaje?

Banana: Ni kweli unayosema lakini huu msalaba ukweli ni wa Kikristo aliniachia marehemu mama yangu mzazi kwa kuwa alikuwa Mkristo.

Star Showbiz: Siri ya mafanikio ya bendi yako maana hapa kati zilifunguliwa nyingi lakini hazikudumu?

Banana: Ni uvumilivu tu na kukubali hasara, pia kuweza kuibeba bendi badala ya bendi kukubeba wewe.

Star Showbiz: Mara nyingi unaambatana na mkeo katika shoo zako, hiyo haileti shida?

Banana: Hakuna tatizo lolote, kwanza kuna mashabiki mbalimbali wa kike ambao huni––fuata kama mashabiki na mpenzi wangu anatambua kama ni mashabiki wangu tu.

Star Showbiz: Kuna uhusiano gani kati ya B Band na Mjomba Band (ya Mrisho Mpoto) maana wasanii wake wanaingiliana kama vile Ismail Kipira ‘Suma’, Nuruel na Beka wa BSS?

Banana: Hizi bendi ni ndugu, kuna sehemu utawasikia hawa na huko kwa Mjomba wapo baadhi kutoka kwangu.

MAKALA: RICHARD BUKOS