

Kivutio cha mwanamitindo na mwigizaji Cara Delevigne, ni nyusi zake.

Mtangazaji wa televisheni, Kim Kardashian, kivutio chake ni makalio murua ambayo wanaume na wanawake lazima wayatazame.
Tumbo la kuvutia lisilo na ‘manyama uzembe’ ndiyo linalozidi kumpa umaarufu mwigizaji, mwimbaji Miley Cyrus.

Umaarufu unaomwongezea mvuto mwigizaji Christina ni, kifua chake kilichopambwa kwa ‘hazina maalum’ inayolazimisha jicho kutazama.

Mwigizaji na mwimbaji Jared Leto kivutio kinachomng’arisha zaidi ni nywele zake ndefu zinazoangukia pande zote za mabega.