×

Simba SC Yaajiri Kocha Mpya Uturuki

Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane.

MABINGWA wa Soka Tanzania, Simba wameonyesha wamepania ku­fanya kweli baada ya kuongeza nguvu ya benchi lake la ufundi.

 

Simba wa­mechukua ko­cha mwingine akiwa ni raia wa Tunisia aitwaye, Adel Zrane. Huyu ni kocha wa viungo ili kuimari­sha fiziki ya kikosi.

 

Zrane anachukua nafasi ya kocha wa viungo wa Simba, Mohammed Habib ambaye aliondoka pamoja na ali­yekuwa kocha mkuu, Pierre Lechantre.

 

Tayari Zrane ameanza kazi na Simba jana kwenye Viwanja vya Milima ya Kartepe hapa Uturuki.

 

Kocha huyo ameanza kazi akishiri­kiana na kocha mkuu mpya wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye pia alianza kazi rasmi nchini Uturuki.

 

Simba ipo hapa Uturuki am­bako imeweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine.