×

ALLEN; TICHA WA ‘UNGENGE’ ALIEMPA UJANJA DIAMOND

2013 kipi-ndi Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platn-umz’ anapi-gania kutoka kimuziki enzi hizo akita-mba na wimbo mmoja wa Kam-wambie, hakuna shabiki aliye-tarajia kama atakuwa staa wa kima-taifa!

 

Leo hii Diamond ni miongoni mwa mastaa wanao-wakilisha siyo Tanzania au Afrika Mashariki tu, bali Afrika nzima. Huwezi kuwataja mastaa watano wanaofanya vizuri Afrika usilitaje jina la Diamond Platnumz kutoka Bongo.

 

Sawa! Ametambulika kimataifa na lugha kubwa anayozungumza awapo nje ya Bongo na mastaa wenzake ni Kingereza, unajua nani aliyesaidia mafanikio hayo? Jibu moja kwa moja litaanzia kwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kuwa amechangia kutokana na kuwa naye katika uhusiano kipindi anatoka kimuziki.

 

Jua na mwambie mwenzako! Wema anaweza kuingia kwa asilimia ndogo sana lakini ukweli unabaki kuwa, nyuma ya ujanja alionao Diamond sasa hivi wa kuongea na mastaa wakubwa kama vile AKA, P Square, Rick Ross, Omarion, Tiwa Savage na Neyo ni mwalimu Allen ambaye jina lake kamili ni Allen Sadick Ngonyani. Yes! Ni mwalimu wa Kingereza aliyefanikiwa ‘kumpika’ Diamond kipindi anatoka 2013.

 

Risasi Vibes limemtimbia hadi kwenye makazi yake na kufanya naye ‘exclusive interview’ na kujua yale ambayo hata wewe msomaji ulikuwa huyajui! Huyu hapa;

 

Risasi: Nini siri ya kuwa mwalimu wa Kingereza?

Allen: Kwanza mimi siyo mwalimu profesheno kwamba nimejifunza ualimu, hapana!Ila nakijua Kingereza na watu huwa wananiita mwalimu kwa kuwa nimekuwa nikiwafundisha.

Risasi: Una elimu gani?

Allen: Elimu yangu ni ya msingi, sekondari na chuo kikuu ila chuo kikuu ndio nimesoma nje ya nchi, nilipata mfadhili nikiwa kwenye meli naenda Zanzibar ndiyo akanipeleka kwao Finland.Picha inayohusiana

Risasi: Nani alikukutanisha na Diamond?

Allen: Alikuwa ni mchumba wake wa zamani anaitwa Penny. Kipindi wana uhusiano nilikuwa rafiki yake mkubwa sasa Diamond alipokuwa anatafuta mwalimu wa Kingereza akaamua anitafute mimi ili nimfundishe.

 

Alinifuata na kuniambia anaomba nimfundishe boyfriend wake Kingereza, nikamuuliza ni nani? Akasema Diamond Platnumz nikaogopa kwa sababu kipindi hicho tayari alishakuwa maarufu. Nikamwambia siwezi, akaniambia utaweza, naomba nisaidie. Basi nikakubali, akanikutanisha naye, akafanya malipo na tukaanza darasa rasmi. Kipindi hicho naanza kumfundisha ndio alikuwa ametoka kuachana na Wema na alikuwa hajui kabisa Kingereza.

 

Risasi: Alikulipa kama shilingi ngapi?

Allen: Alikuwa ananilipa vizuri sana ila siwezi kutaja ni kiasi gani kwa sababu sio vizuri ila kwa kukurahisishia tu alikuwa ananilipa chini ya milioni.

 

Risasi: Ulikuwa unaridhika kwa kiasi alichokulipa?

Allen: Nilikuwa naridhika sana tena sana kwa sababu alikuwa ananilipa mshahara na kuniongezea kiasi kingine juu. Hii yote ni kwa sababu alikuwa anasema ananielewa vizuri.

Risasi: Ulimfundisha kwa muda gani?

Allen: Hatukuchukua zaidi ya miezi mitatu.

Risasi: Vipi uelewa wake ulikuwaje?

 

Allen: Diamond ni mtu ambaye ni mwepesi kuelewa mno, yaani anaelewa haraka hadi nilikuwa nahisi kama alikuwa anajifanyisha kutokujua Kingereza. Ilikuwa nikimfundisha leo kesho yake anakuwa ameshaelewa kila kitu na ananiambia vizuri yaani hakosei aisee! Naweza kusema nilikuwa nainjoi kumfundisha.

Risasi: Bado mpaka leo mnawasiliana?

Allen: Tunawasiliana vizuri tu, baada ya kumfundisha karibu familia nzima wakawa marafiki zangu na mpaka leo ni marafiki zangu, sasa hivi namfundisha dada yake anaitwa Esma.

Risasi: Kipindi ulichomfundisha Diamond uligundua nini?

Allen: Ni kijana mzuri sana, mbali na kumfundisha lakini ni rafiki pia hata nikiwa na shida nikimwambia ananisaidia iwe kipesa au vitu vingine ananisaidia. Halafu alikuwa ananiambia ticha mimi ni mwanafunzi wako ukiwa na shida niambie wala usiwe na wasiwasi.

Risasi: Ni changamoto zipi ulikutana nazo?

 

Allen: Kubwa ni kwamba Diamond alikuwa busy sana! Yaani tunaweza tukapanga kusoma saa kumi na moja kila siku lakini unakuta wakati mwingine amechelewa kuja kwenye kipindi kwa sababu ya mambo mengi kama vile show, kwa hiyo inanifanya kusimamisha darasa kidogo mpaka atakaporudi ndiyo niendelee naye.

 

Risasi: Lakini kuna maneno kuwa Wema alihusika kumfundisha?

Allen: Mimi ndiyo nimekaa naye chini na kumfundisha Kingereza siyo Wema wala mwingine, nimemkuta Diamond yupo chini kabisa kwenye Kingereza, hata mara ya kwanza namwambia ajitambulishe kwa Kingereza alikuwa hajui chochote na mimi nimeanza kumfundisha kipindi kashaachana na Wema yupo na Penny, sasa inawezekana vipi kuwa Wema ndiye aliyemfundisha?

 

Risasi: Kuna staa mwingine umewahi kumfundisha?

Allen: Wengi tu akiwemo Chege ila bahati mbaya darasa letu halikwenda sawa kwa sababu mimi ndio ambaye nilikuwa bize sana na pia nimebahatika kufundisha WCB wote Diamond ndiyo alilipia.