
NDUGU, jamaa na marafiki wamefika kuungana na waombolezaji na wafiwa wote nyumbani kwa marehemu Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric James Shigongo, Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia leo.

Bi. Kapela amefariki dunia alfajiri ya leo Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za mazishi zitafanyika.

Kwa niaba ya wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group, tunapenda kutoa pole kwa familia ya Shigongo, pole kwa ndugu jamaa na marafiki, pole kwa wafanyakazi wenzetu kwa kupata pigo la kuondokewa na mpendwa wetu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe, AMEN!





