Mambo yanazidi kukolea katika Shindano la Tusua Maisha na Global, ikiwa ni droo ya nane ambapo Jackson Bwire, msomaji kutoka Ukerewe, Mwanza, ameibuka kidedea kwa kujishindia pikipiki mpya kutoka Global.
Katika droo hiyo iliyochezeshwa Jumanne ya Agosti 14 na kurushwa mubashara na kituo cha runinga cha Global TV Online, Jackson ambaye anajishughulisha na kuuza mbao, aling’ara sambamba na wasomaji wengine wawili, ambao ni Nobert Benjamin wa Nyamagana Mwanza aliyejishindia dinner set na Gasper Ndimbo, mkazi wa Miseko, Mkuranga aliyejishindia jezi.
Namna ya kushiriki ni rahisi sana cha kufanya nunua gazeti lako lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Amani, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya jinsi ya kushiriki.
Itume namba maalum inayoonekana juu ya kuponi hiyo kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kiopande cha kuponi yako au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukua zawadi.