×

UWT YASISITIZA KUSIMAMIA VIPAUMBELE VYAKE

Katibu Mkuu wa UWT-Taifa, Mwl. Queen Mlozi  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

Umoja wa Wanawake Watanzania (UWT) umezungumzia namna ulivyojipanga kuhakikisha unasimamia vipaumbele vyake katika kipindi cha mwaka 2018-2019 ambavyo ni pamoja na kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa  katika huduma za kijamii kama vile maji, elimu na afya ya mama na mtoto.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ndogo za CCM Mtaa wa Lumumba, Katibu Mkuu wa UWT-Taifa, Mwl. Queen Mlozi amesema kuwa kazi ya umoja wa wanawake ni kuhakikisha unajiimarisha kiuchumi, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha vilivyopo kuanzia ngazi ya kata hadi taifa na kubainisha mali zote za UWT.

Mbali na hayo, ameeleza kuwa umoja huo utaendelea kutoa elimu kwa watoto wa shule za msingi juu ya madhara ya mimba za utotoni na jinsi wanavyokosa fursa za kujiendeleza kielemu kutokana na  kujiingiza katika masuala ya mapenzi wangali shuleni.