×

Lowassa Ampa JPM Miaka 10, Sumaye Atia Neno – Video

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,  amemsifia Rais John Magufuli kwa jitihada za kuleta maendeleo makubwa nchini tangu aingie madarakani na kwamba pindi akiendelea kuwa madarakani kwa miaka kumi nchi itakuwa imepiga  hatua kubwa katika maendeleo.

 

Lowassa aliyekuwa waziri mkuu mwaka 2005 hadi 2008 ametoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) yaliyofanyika kitaifa mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

 

“Amani ndio msingi anaoutumia mheshimiwa Magufuli leo kuongoza nchi yetu, kuleta mshikamano na umoja, nampongeza amefanya kazi nzuri sana. Kama Rais Magufuli ataachiwa akamaliza miaka yake 10 nchi hii itabadilika,  itakuwa kubwa na yenye maendeleao makubwa sana.  Kwa hiyo ninaomba tumuunge mkono tumsaidie ili nchi yetu izidi kwenda mbele,”  amesema.

 

Lowassa alikihama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mwaka 2015 na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipitishwa kugombea urais mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu, lakini baadaye Machi Mosi, 2019, alirejea CCM.

 


Wakati huohuo, akizungumza katika maadhimisho hayo waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye,  ambaye alikuwa Chadema na hivi karibuni kuachana na chama hicho amesema:

 

“Leo tunasherekea uhuru ambao tuliupata wakati huo tukiwa bado tatizo la kiuchumi lakini tunaamini kwa kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli tutajikomboa. Taifa letu bado ni tegemezi lakini nina imani utatutoa huko. Kuna kazi kubwa inafanywa na serikali lakini tuna kazi kubwa ya kupata uhuru wa kiuchumi kuondokana na utegemezi,” amesema.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

Leave a Comment