×

Wasomaji Wafurahia Bei Mpya ya Sh. 500 ya Spoti Xtra

Wauza nyama wa Tabata-Segerea, Dar es Salaam wakilifurahia Spoti Xtra.

GAZETI la Spoti Xtra limekuja katika ujio mpya unaohusisha  punguzo la bei  ambapo kuanzia leo (Jumapili) linauzwa kwa Sh. 500 tu badala ya Sh. 800 iliyokuwepo awali na litakuwa linatoka mara mbili kwa wiki — Alhamisi na Jumapili.

Muuza mihogo maeneo ya Vingunguti akijinafasi na Spoti Xtra.

Uzinduzi wa punguzo la bei umefanyika leo ambapo timu ya gazeti hilo la Spoti Xtra ilitembelea wasomaji wake  maeneo ya  Tabata-Kinyerezi, Segerea,  Vingunguti, Ubungo, Mwenge na sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo magazeti yalitolewa bure.

Muuza matunda wa Baracuda, Tabata,  akufuatilia kwa makini uhondo wa Spoti Xtra.

Baada ya timu ya promosheni ya Spoti Xtra kutembelea wasomaji sehemu hizo, wasomaji hao walitoa pongezi kibao kwa maombi waliyoyatoa kuhusu kupunguziwa bei kwa gazeti hilo.

Ofisa Masoko wa Spoti Xtra, Jimmy Haroub (kushsoto) akijibu maswali ya wasomaji kwenye mgahawa wa Juice Kingdom wa Tabata-Segerea.

Ili kujishindia zawadi hizo, msomaji anatakiwa kununua gazeti la Spoti Xtra siku ya Alhamisi na Jumapili  ambapo utatakiwa kujaza kupoeni iliyomo ndani ya gazeti hilo kwa kufuata maelekezo yaliyomo.

Ofisa Masoko wa Usambazaji na Masoko, Anthony Adam (kushoto) akitoa maelekezokwa msomaji wa Spoti Xtra.

 

Uongozi wa Spoti Xtra umedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ya kuliboresha gazeti na wasomaji wake wakae mkao wa kupata burudani ya kutosha.

Wasomaji wa Tabata-Matumbi wakifurahia habari zilizosheheni katika Spoti Xtra.
Ofisa Usambazaji, Anthony Adam (kushoto), akizungumza jambo na msomaji wa Spoti Xtra.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL