
MWIGIZAJI na komediani maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewataka wasanii wote kwa jumla bila kujali wa muziki au filamu kuwa pamoja kumuombea msamaha msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama ambaye mpaka sasa yupo kituoni kwa kosa la uharibifu wa mali ya umma. Mau na mtangazaji wa Clouds, Soud Brown wanadaiwa kusambaza video mitandaoni ikionesha watu wanaokanyaga noti za shilingi elfu kumi. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Steve alisema anawaomba wasanii waungane kumuombea msamaha Maua kwani ni mwenzao.
“Msanii yeyote ni kioo cha jamii, chochote atakachokifanya kinaweza kuwa na faida au hasara, kwa kile walichokifanya, mimi na wasanii wote bila kujali wa muziki au wa filamu tuwaombee kwa vyombo vyote husika kwa kuwa natumaini wamejifunza na naomba tu wapewe dhamana,” alisema Steve.