×

WAYNE ATIMIZA MIAKA 36, AACHIA NGOMA YA ‘THA CARTER V’

RAPA Mmarekani, Lil Wayne ameadhimisha ‘bethidei’ yake ya mwaka wa 36 na kuachia ngoma yake ya  Tha Carter V, katika hafla iliyojaa mastaa mbalimbali katika Hubble Studio, Los Angeles, usiku wa kuamkia jana.

Katika tukio hilo, Wayne anayejulikana pia kama Weezy, alijumuika na nyota maarufu katika kufurahia  siku aliyoiita  “Wayne’s World”  ambapo kulikuwa na mastaa kibao wakiwemo Stevie Wonder, Chris Brown, Big Sean, Wiz Khalifa, Ashanti, Tiffany Haddish, Timbaland, Ray J, Rae Sremmurd, Trippie Redd, Trey Songz, na binti yake, Reginae.

Miongoni mwa viburudisho katika ‘mnuso’ huo  vilikuwa vyakula na vinywaji mbalimbali maarufu, peremende, bangi, na kadhalika.  Pia kulikuwepo vifaa vya mchezo wa ‘skate’ ambao anaupenda rapa huyo.

 Pia ngoma yake ya Tha Carter V iliyokuwa inasubiriwa, ilitoka ikiwajumuisha Kendrick Lamar, Nicki Minaj, Travis Scott, XXXTentacion, Snoop Dogg, Ashanti,  na wengine.