×

Tattoo za Wawa zina maana nyingi

HUENDA beki wa kigeni wa Simba, Pascal Wawa ndiye mchezaji mwenye michoro mingi mwilini ‘tattoo’ kati ya wachezaji wanaocheza katika Ligi Kuu Bara ambapo beki huyo ameweka bayana maana yake.

 

Wawa aliyesajiliwa msimu huu ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi ana michoro kibao kuanzia miguuni na mikononi.

,

Nyota huyo wa zamani wa Azam FC ameliambia Spoti Xtra kwamba; “Hii sura ya mwanamke unayoiona ni sura ya mke wangu anaitwa Martine Wawa, nampenda sana ndiyo maana nimemchora lakini pia hii tattoo ya kwenye bega yenye sura ya mtoto nimeamua kumchora mtoto wangu wa kiume anaitwa Noah, nimejaribu kuonesha hisia zangu kwa kutumia tattoo.’

 

Wawa amechora sura ya mke wake kwenye paja la mguu wa kushoto huku pia akichora sura ya mwanae kwenye bega lake la kulia.

ISAYA MBENA, DAR ES SALAAM