
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Giles Muroto, amesema Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na Operesheni ya kusaka wahalifu ambapo mpaka sasa wanawashikilia wahalifu zaidi ya 100 akiwemo kijana mmoja aliyekuwa akifanya utapeli kwa kujifanya Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).