Global Education Link Ltd, Agency, ndiyo wakala bora zaidi nchini Tanzania wa kusajili wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchi za nje. Wakurugenzi wake wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchi za nje, hivyo wana uzoefu na maarifa halisi ya maisha ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu nchi za nje.
Mnamo miaka mitatu iliyopita, wakala huyo ameweza kuhudumia wanafunzi zaidi ya 2,000 walionufaika na mipango yao ya kuwatafutia nafasi za kusoma vyuo vikuu nchi za nje.
Global Education Link Ltd huhakikisha kila mwanafunzi anapata mafanikio katika masomo yake kwa kushughulikia matakwa na mahitaji yake ambapo wanahakikisha pia mwanafunzi anapata fursa ya kujifunza utamaduni mwingine na jinsi ya kuweza kuishi katika mfumo mpya wa maisha wakiwa huko.
Ili kupata fursa hii, muombaji lazima awe amemaliza elimu ya juu ya sekondari (high school) ambapo vyuo vikuu vingi husika vinapenda kuchukua wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la C na kuendelea, kwa wanafunzi wanaotegemea kuchukua shahada ya kwanza.