×

Mwili wa Isaac Gamba Wawasili Viwanja vya UTPC Mwanza Kuagwa – Pichaz

MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba umewasili katika Viwanja vya Ofisi za Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari (UTPC) jijini Mwanza kwa ajili ya taratibu za kuagwa.

Mwili wa Gamba ambao uliwasili jana nchini na kuagwa katika Hospitali ya Lugalo jijini Dae re Salaam kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Mwanza, umewasili jijini humo leo Jumanne, Oktoba 30, 2018 asubuhi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, wanahabari na waombolezaji wengine wameshawasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ibada ya kuaga.

Baada ya kuagwa jijini Mwanza, mwili huo utasafirishwa kwenda nyumbani kwao wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

MAJONZI: Mwili wa Isaac Gamba ulivyowasili Mwanza