
MISS Morogoro 2018, Amne Kubri amefunguka kuwa, juisi ya Kingdom inayotengenezwa kwa matunda halisi Bongo, ina utamu uliopitiliza hivyo anawashauri warembo wenzake pamoja na Watanzania kwa ujumla kuitumia ili wajionee utofauti.

Akizungumza na mwanahabari wetu akiwa katika tawi la Juice Kingdom, Tabata Segerea hivi karibuni, Amne alisema, ameshawahi kunywa juisi nyingi kabla ya Juice Kingdom lakini baada ya kuinywa katika maeneo matatu tofauti (Tabata, Africasana na Mikocheni), amegundua ina ubora wa hali ya juu.

“Ni juisi tamu, nzuri na bahati nzuri nimeshuhudia hata namna inavyotayarishwa. Haichanganywi na kemikali zozote zaidi ya matunda halisi,” alisema Amne.

Naye Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron Julius, alisema mbali na mrembo huyo, juisi yake imekuwa ikipendwa na mastaa wengi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na kutengenezwa kwa matunda halisi na kufungwa vizuri katika chupa zake.

“Ni juisi inayofaa kunywewa na familia, baba mama watoto, watu mbalimbali. Tupo Tabata Segerea, Sinza Afrikasana na Mikocheni, nawasihi Watanzania wajaribu bidhaa zetu, wajionee utofauti,” alisema Zabron.