Naibu waziri wa maliasili na utalii Constantine Kanyasu ametoa msaada wa vyakula katika vituo vitano vinavyolea watoto yatima katika jimbo la Geita mjini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za krismas na mwaka mpya.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Naibu waziri Kanyasu katibu wa mbunge huyo Marium kaka amesema Naibu waziri amekuwa na desturi hiyo kila mwaka.
Kwa upande wao watoto wanaolelewa katika vituo hivyo wamemshukuru naibu waziri Constantine Kanyasu kwa moyo huo wa kuwakumbuka katika kipindi hiki cha sikukuu.
Baadhi ya vituo vilivyopata msaada huo ni moyo wa huruma, bright light,meriko,mema house na mama mkubwa