Kilo 323.6 za dhahabu zenye thamani ya shilingi trillion 3 zimekamatwa zikitoroshwa kinyemela kwa magari mawili kwenda kuuzwa nchi jirani kupitia Mkoa wa Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama ya Mkoa, John Mongela amelipongeza jeshi la polisi kwa kubaini utoroshwaji wa rasilimali ya nchi.