Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ameagiza Mamlaka za kinidhamu kuwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Uyui wanaosimamia Sekta ya Kilimo na ushirika kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yao ikiwemo kuwaacha wakulima waendeshe kilimo cha Pamba pasipo kufuata kanuni za kilimo cha zao hilo.