×

RC MAKONDA: DAR Ruhusa Kufanya Kazi Saa 24, Hakuna Kulala – VIDEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaama una mpango wa kuhakikisha wafanyabiashara wote wa mkoa huo wanafanya biashara zao saa 24 ili kila mwananchi apate fursa ya kufanya mahitaji yake pale anapoona muda.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 8, amesema kuwa kama ambavyo rais alikwisha kusema kuwa Jiji la Dar es Saalaam ni la kibiashara hakuna budi mkoa wa kutimiza adhma hiyo ili kuliweka katika hali zaidi ya kibiashara na mpango uliopo ni kuhakikisha unakutana na wafanyabiashara wote kuzungumzia juu ya ufungaji wa kamera za kisasa kwa ajili ya ulinzi zaidi ili mkoa wa uwe wa kibiashara.

 

Aidha Katika suala la miundombinu ya maji Makonda ameeleza kuwa zaidi ya billion 5oo zimekwishakutengwa kuhakikisha kuwa maji yanapatikana na jitihada zaidi zinaendelea na sehemu ambayo hakuna maji visima vya maji vinachimbwa. KUHUSU suala la Elimu RC Makonda amempongeza rais magufuli kwa kuwezesha utoaji Elimu bure kwa wanafunzi kote nachini.

 

KUHUSU suala la Elimu RC Makonda amempongeza rais magufuli kwa kuwezesha utoaji Elimu bure kwa wanafunzi kote nachini. Katika kipindi hiki cha mwaka wa Masomo wa 2019 mkoa wa Dar es Saalaam umejipanga kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu mtihani anaripoti tayari kwa kuanza na Masomo na upungufu wa vyumba vya madarasa uliokuwepo unashughulikiwa ili kila mtoto apate elimu.

 

Ametoa raia kwa wazazi ambao hawata peleka watoto wao shule watashughulikiwa na sheria stahiki zitachukuliwa.