Kila Unapofanikiwa kuamka asubuhi ukiwa na afya njema unatakiwa kumshukuru Mungu kwani wapo ambao kila wanapoamka tu wanameza dawa au kwenda hospitali.
Katika kipindi cha ushuhuda wiki hii tunae Mwanadada, Asia Mustapha, ambaye ukiliona tabasamu usoni mwake lilivyojaa hautaweza kuamini kama anaishi bila kuwa na figo hata moja kwa zaidi ya miaka 12 sasa lakini ukimuona ni kama mzima wa afya kwa jinsi ambavyo amekubaliana na hali yake na anamshukuru Mungu.