Ni usiku wa Chekelea Stand Up Comedy, katika ukumbi wa Kebbys Hotel iliyopo Mwenge, ambapo wasanii kibao wa vichekesho akiwemo Oscar Nyerere, Black Passy, JK Comedian na wengine wengi wanafanya shoo ya kuwavunja watu mbavu.
Mgeni rasmi katika usiku huu ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza, aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza.
