×

MWILI WA KIBONDE ULIVYOAGWA, WATANGAZAJI CLOUDS VILIO! – VIDEO

Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, marehemu Ephraim Kibonde, umeagwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa serikali, Wasanii na watangazaji wenziye.

Baada ya kuagwa mwili huo unatarajia kuzikwa leo Jumamosi saa 9, alasiri katika makaburi ya Kinondoni.

Kibonde ambaye alikuwa mshehereshaji kwenye msiba wa Ruge amekutwa na umauti katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza Machi 6, 2019.

Mtangazaji huyo alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliomsindikiza Ruge hadi katika maziko yake kijiji cha Kiziru, Bukoba.