×

JPM: Huwezi Kuendesha Viwanda kwa Dizeli – Video

Rais Dkt. John Magufuli amezindua mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme ya Kilovolt 220 kutoka Makambako hadi Songea leo, Jumamosi April 6, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Magufuli amesema;

“Leo ni siku ya historia kubwa kwa mkoa wa Ruvuma, suala la umeme lilikua tatizo kibwa tulikua tunatumia majenereta, tunawashukuru Sweeden kwa kutoa fedha za wa walipa kodi za wananchi wao kutusaidia.. hawa ni marafiki wa kweli.

 

“Mradi huu una faida nyingi ikiwemo kusaidia kuokoa billion 9.8 ambazo zilikuwa zikitumika kuzalisha umeme wa mafuta na mnafahamu katika nchi ya Tanzania wajanja ni wengi sitaki kuwatuhumu watu wa hapa hasa wa Tanesco,

 

“Ni lazima tuweke uwekezaji wa kutosha katika umeme maana nchi yoyote inayotaka kujikomboa katika uchumi lazima iwe na umeme. Hatuwezi tukashindana na nchi nyingine kwasababu wao wanatengeneza bidhaa za bei ya chini na sisi tunatengeneza bidhaa za bei ya juu mwisho zitadoda kwenye soko halafu tutakuwa tunawatengenezea wao ajira.

 

“Huwezi kuendesha viwanda kwa dizeli, na ili uendeshe viwanda lazima umeme uwe wa bei ya chini. Mahitaji ya umeme katika nchi yetu ni makubwa na yataendelea kuwa makubwa kwasababu tumeamua kuifanya kuwa ya viwanda kwa bahati mbaya bei ya umeme kwa unit katika nchi yetu ni kubwa sana.

 

“Nimefurahi kumuona balozi wa Sweden hapa ili aone kuwa fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo hakuna rushwa kwani azma na dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuifanya nchi yetu kuwa na umeme wa kutosha na wa bei nafuu, Sweden ni marafiki wa kweli tangu enzi za baba wa taifa na hili ninalisema kwa ukweli na uwazi na tunawaomba waendelee kutupa ushirikiano katika masuala mengine.

 

“Sikuja hapa kuzungumza mambo mengi nitoe wito kwa watendaji wa Tanesco endeleeni kuulinda huu mradi na kwa watumiaji wa mradi huu endeleeni kuutunza na kuutumia vizuri kwa manufaa ya nchi yetu katika kuleta manufaa ya kweli,” amesema Rais Magufuli.

MSIKIE MAGUFULI HAPA AKIFUNGUKA