Rais Dkt.John Pombe Magufuli amempandisha cheo Kanali Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali, zoezi ambalo limetekelezwa mara moja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na kumvisha vyeo Luteni Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali katika Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.
Rais Magufuli amefanya tukio hilo leo Jumamosi, Aprili 13, 2019 wakati akizindua ofisi za Serikali katika Mji wa Kiserikali wa Mtumba, Makao Makuu ya Nchi Dodoma ambapo hatua hiyo imetokana na kufanya kazi bora katika kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa Serikalini.
Rais Magufuli amewaajiri vijana wa JKT walioshiriki kujenga Nyumba 10 za Wizara Katika mji wa serikali Dodoma walioshiriki kujenga Nyumba 41 za wafanyakazi wa ikulu, walioshiriki kujenga ukuta wa ikulu Chamwino na waliopo kwenye Ghala la chakula la Mlale.