
Bodi ya Filamu nchini kwa kushirikiana na wadau wa filamu Juni 26, 2020 wamezindua kanuni za ubora wa filamu ambazo zitaoneshwa kwenye majumba ya filamu nchini.
Bodi hiyo kwa kushirikiana na wasanii pamoja na wamiliki wa majumba na kuonesha sinema wameanzisha utaratibu wa kuonesha sinema hizo kwenye majumba hayo kama ilivyo siku za nyuma.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiango Kilonzo amesema utaratibu huo utaweza kuwanufaisha waandaaji wa filamu hizo, wasanii, wamiliki wa majumba hayo pamoja na serikali kwa kupata kodi.

Dkt. Kilonzo amesema katika mpango huo wameunda kamati ya kuzikagua filamu hizo ambapo Mwenyekiti Abdullah Mohammed ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwa na wajumbe wengine akiwemo Ahmed Ulotu maarufu kama Mzee Chillo na wengineo.

HABARI/PICHA: WAANDISHI WETU