×

Mazishi ya Seth Bosco, Vilio na Majonzi Makaburi ya Kinondoni – Video

SIMANZI, vilio na majonzi vimetawala wakati mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco ukizikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, Desemba 9, 2019.

Mama mkubwa wa marehemu, Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ alionekana kuishiwa nguvu mara kwa mara huku akilia kwa uchungu kutokana na kumpoteza mwanaye huyo aliyekuwa msaidizi wake mkubwa tangu kifo cha Kanumba.

Hata hivyo watu wa karibu na mama huyo wamejaribu kufariji na kumsihi awe mvumilivu katika kipindi hiki kigumu anachopitia cha kupoteza watoto wake aliyokuwa akiwategemea kumsaidia katika maisha yake ya kila siku.

Seth ambaye alifariki juzi Jumamosi, Desemba 7, 2019 baada ya kuugua kwa muda kutokana na kupooza wakati akiwa kanisanai, amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walioungana na familia ya marehemu katika msiba huo.

 

Leave a Comment