
ALIYEKUWA kocha mkuu wa timu ya soka ya Nkana ya nchini Zambia, Beston Chambeshi, amevunja mkataba na klabu hiyo katika kukamilisha mchakato wa kujiunga na klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Kocha huyo alijiunga na Nkana mnamo Julai 2016 ambapo ilishika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu nchini humo inayojulikana kama FAZ/MTN Super League.
Alifanikiwa kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kufika fainali za Kombe la Barclays mwaka 2017 na kufikia robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Rais wa Nkana, Everisto Kabila, amemshukuru Chambeshi kwa kazi aliyoifanyia klabu hiyo na kumtakia kila la heri aendako.
Wakati huohuo, kocha Manfred Chabinga ataendelea kukaimu nafasi ya kocha mkuu hadi patakapotolewa uamuzi mwingine.
Na JOHN SAKALA
