×

LIVE: Mwili wa Bilionea Mufuruki Ukiagwa JNICC Dar

MWILI wa bilionea Mtanzania na Mwenyekiti mwanzilishi wa Jukwaa la Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group, Ali Mufuruki,  unaagwa leo Desemba 10, 2019,  katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, baada ya kuwasili jana kutokea Afrika Kusini.

 

Mufuruki alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili ya Desemba 08, 2019,  akiwa Afrika Kusini, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimkabili katika Hospitali ya Morningside, jijini Johannesburg.

 

Viongozi mbalimbali wa kitaifa na wafanyabiashara wameshiriki kuuaga mwili huo.  Watu mbalimbali walieleza kuguswa na kifo cha mfanyabiashara huyo, akiwemo Rais John Magufuli.

 

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amewasili katika ukumbi huo kuungana na mamia ya wananchi, taasisi mbalimbali na jumuiya za wafanyabiashara. Viongozi wengine walioelezea hisia zao kwa kifo hicho ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

 

FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA

Leave a Comment