
JAMANI… jamani habari hizi zinashtua na kuhuzunisha wengi waliotamani kuiona kapo yao ikidumu miaka mia nane.
Lakini habari mbaya zinazosambaa mitandaoni zinadai kuwa staa wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ ameachana na mwandani wake, Anerlisa Muigai, yule mwanamke bilionea wa nchini Kenya.
AMANI LINA MAJIBU YA BEN POL
Hata hivyo Gazeti la AMANI limezungumza na Ben Pol muda mfupi uliopita, akafunguka ya moyoni na kuahidi kurudi nyumbani Bongo.
Maneno ya mitandaoni tangu kumekuwa leo Jumatano, yanaeleza kuwa, Ben Pol na Anerlisa hawako poa na yale mahaba nining’inize ya awali yameota mbawa.
CHATTING ZA HAMISA
Sosi wa karibu wa wawili hao amemwaga ubuyu kama wote kwa wananzengo kuwa kimenuka vibaya mno baada ya Anerlisa kunasa chatting za Ben Pol za kimahaba na mwanamke mmoja maarufu Bongo aliyetajwa kwa jina la Hamisa.
Hata hivyo, haikufafanuliwa sana kama ni huyu Hamisa Mobeto au ni Hamisa mwingine.
Unaambiwa bibie Anerlisa baada ya kupata ushahidi wote kiganjani, kwanza akamtoa Ben Pol kwenye kundi la wafuasi wake katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Inasemekana kwamba, kutokana na aibu, Ben Pol akajitoa kwa muda mitandaoni hasa kwenye Instagram ili kupisha upepo mbaya upite.
ISIWE KWELI MAANA…
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki na wafuasi wao wanaendelea kumuomba Mungu habari hizo za kuachana kwao zisiwe za kweli.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimtafuta Ben Pol na kumuuliza kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na Anerlisa huku Hamisa akitajwa ambapo alisema amesikia habari hizo.
Lakini Ben Pol amesisitiza kuwa, yeye na Anerlisa wapo vizuri na hayo ni maneno ya watu ambao wanataka uhusiano wao uvunjike.
“Ni kwamba kuna watu wanapenda kuzusha vitu hasa wakigundua kuwa uhusiano wetu upo strong (imara). Ukweli ni kwamba mimi na mchumba wangu tuko vizuri kwa asilimia mia na sijawahi kumchiti.
NARUDI NYUMBANI SOON
“Kwa nini nifanye hivyo wakati nimemchagua mwenyewe na ninampenda pia?
“Narudi nyumbani Bongo soon kwa ajili ya projekti zangu mpya,” amesema Ben Poul akiwa nje ya nchi.
Saa kadhaa baada ya ishu hiyo kusambaa mitandaoni, Anerlisa alifunguka kupitia Insta Story yake ambapo aliandika; “Mara nyingi mpenzi wangu amekuwa akiniambia pale inapotokea maneno ya kutengeneza, nisiwe mwepesi wa kujibu kwani ni mambo ya kupita. Najisikia kubarikiwa.”
TUJIKUMBUSHE
Uhusiano wa Ben Pol na Anerlisa ulianza yapata mwaka mmoja uliopita ambapo katikati ya mwaka huu walitimiza taratibu zote za kimila na kinachosubiriwa ni harusi ya kukata na shoka kutokana na utajiri anaotajwa kuwa nao binti huyo.
Mshtuko Dar! Vijana Wachinja, Wala Nyama Mbichi ya Paka