DAR: Mwanamama anayekisanua kwenye Bongo Muvi, Irene Uwoya, amefunguka kuwa, hawezi kuwa na noma akimuona mpenzi wake anamkisi mwanamke mwingine au kumuita majina ya kimahaba, lakini kitakachomkosesha uvumilivu ni kuona akisalitiwa.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya alisema; “Mimi naona ni kawaida tu kama watu ambao wana urafiki kukisi ni vitu vya kawaida tu hakuna kikubwa hapo haimanishi chochote hata kumwita mtu darling ni sawa tu.
“Hata mimi mtu yeyote naweza kumuita hivyo,” alisema Uwoya.
Alisema kinachoweza kumshinda kuvumilia, ni kitendo cha mwanaume wake kumsaliti.
“Kwangu mimi mwanaume wangu akimkisi mwanamke itategemea, unajua kuna kisi zinatofautiana, ukifanya hivyo katika hali ya urafiki inaonekana na ukifanya katika hali ya mapenzi inaonekana pia, mimi nitachukulia kitu cha kawaida cha urafiki hakuna tatizo ila akinisaliti siwezi kuvumilia,” alisema Uwoya.
Stori: NEEMA ADRIAN, Ijumaa