×

Wema Amtolea Povu Mobeto

MWANADA SHOSTI wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ametoa povu si la nchi hii, kisa staa mwenzake, Hamisa Mobeto ‘Misa’.

 

Wema ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, anashangaa ni kwa nini watu wanapenda kuchonga sana akimposti Misa kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumwambia ni mke mwenzake. Jambo ambalo linamkera ile mbaya.

 

“Watu wanataka nisimposti Misa? Kwani ni mke mwenzangu? Nina uhuru wa kuposti chochote kwenye ukurasa wangu,” amesema Wema ambaye ‘ukewenza’ na Misa unatokana na kuwa wote ni ‘maeksi’ wa Mondi.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Leave a Comment