×

Rais JPM: Nimechoka… Kazi Hii ni Mateso – Video

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa chama hicho ni kiwanda kinachopika viongozi bora, hivyo hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kinyume na Katiba ya chama hicho na Katiba ya nchi.

 

Mhe. Rais Magufuli amesema majukumu ya Urais ni mazito na kwamba hata yeye hakutarajia kama angekutana na uzito wa majukumu anaokutana nao hivi sasa.

 

Ametoa kauli hiyo alikuwa akizungumza katika vikao vya Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyofanyika Jijini Mwanza.

 

Leave a Comment