
Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SCAP. Muliro Jumanne Muliro, leo Jumatatu Septemba 23, 2024 amesema Jeshi la Polisi limewakamata watu 14 wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chadema ambao ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu pamoja na Godbless Lema.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watu hao wanaendelea na mahojiano.
