×

Polisi Yawaonya Madereva Kipindi cha Sikukuu

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP,  Fortunatus Muslim,  akizungumza na madereva wa mabasi yanayokwenda mikoani.

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, Fortunatus Muslim,  amewataka madereva kuwa waangalifu katika kuhakikisha usalama wa abiria hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na uzoefu wa huko nyuma kwamba kipindi kama hiki hutokea ajali nyingi.

Pia aliwataka kuzingatia suala la afya na kuwasisitiza kutosimamisha magari sehemu zisizo rasmi kwa ajili ya abiria kujisaidia, akisema suala hilo maarufu kama ‘kuchimba daw’a ni kosa kisheria na sio salama kwa wananchi kujisaidia vichakani.

Aliongeza kwamba hilo linaweza kuwasababishia ajali kutokana na madereva kusimamisha magari maeneo ambayo si salama, ambapo, badala yake,  amewataka kusimamisha magari maeneo ambayo yamejengwa vyoo na yameandaliwa rasmi kwa abiria kupata huduma hiyo.

PICHA NA JESHI LA POLISI

Leave a Comment