×

Muuguzi Mbaroni kwa Kumbaka Mjamzito Akijifungua – Video

 

MUUGUZI wa Kituo cha Afya Mamba, mkoani Katavi, Abednego Alfred (32), anadaiwa kumbaka mjamzito aliyekuwa kwenye chumba cha kujifungulia, akisubiri kujifungua.

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 18, saa mbili usiku, katika kituo hicho cha afya.

 

Alisema siku ya tukio, mwanamke huyo alipatwa na uchungu na kwenda kupata huduma ya kujifungua kwenye kituo hicho cha afya huku akiwa amesindikizwa na mama yake mzazi na kwamba mjamzito huyo alipokelewa kituoni hapo na mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa zamu kwenye wodi hiyo ya kujifungulia.

 

Kamanda Kuzaga alieleza, wakati mtuhumiwa akimpatia huduma ya uzazi mgonjwa, alihisi hali isiyo ya kawaida katika sehemu zake za siri hali iliyomfanya ashtuke.

 

Alieleza kuwa mgonjwa huyo alijiinua na kumuona muuguzi Alfred akiwa anamwingilia katika sehemu zake za siri bila kujali hali aliyokuwa nayo.

 

Kamanda aliendelea kueleza mgonjwa baada ya kuona hivyo, aliinuka kitandani na kwenda moja kwa moja kutoa taarifa kwa mama yake mzazi (jina linahifadhiwa) ambaye naye alitoa taarifa kwa uongozi wa kituo hicho cha afya.

 

Vile vile, Kamanda alisema mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho aliondoka ndani ya chumba hicho cha kujifungulia na kisha kukimbia na kutokomea kusiko julikana. Hata hivyo polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumkamata.

 

Alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

 

DAKTARI AMBAKA MJAMZITO AKIMZALISHA, RPC ASIMULIA | TBC1

Leave a Comment