×

Simba Queens wapo Dar, Yanga kukinukisha Iringa Leo

 

Kocha Msaidizi wa Yanga Princess, Nassoro Mukhsin aliliambia gazeti hili kuwa: “Huu ni mchezo muhimu kwetu kusahihisha makosa tuliyofanya katika mchezo uliopita dhidi ya Simba Queens, naamini ushindi utapatikana.”

 

Kwa upande wa kiungo wa kimataifa wa Burundi anayekipiga Simba Queens, Joelle Bukuru, alisema: “Muhimu ni pointi tatu katika kila mchezo tutakaocheza mbele yetu, tupo nyumbani na tutajaribu kucheza vizuri ili tupate pointi tatu.”

JKT Queens watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ruvuma Queens, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea, michezo mingine itakayochezwa leo ni Mlandizi Quees dhidi ya Kigoma Sisterz, TSC Queens na Baobab Queens, huku Alliance Girls wakicheza dhidi ya Tanzanite.

Leave a Comment