×

Nondo Ashinda Rufaa Kesi Yake ya ‘Kujiteka’

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa, imemuachia huru aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo, baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri  baada ya kutoridhishwa na hukumu yake aliyoshinda mwaka 2018.

 

Abdul Nondo ameachiwa jana Desemba 23, 2019, ambapo mahakama imesisitiza kuwa hana hatia na kwamba hoja za rufaa za upande wa serikali, zimeonekana kutokuwa na mashiko.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mara baada ya kushinda rufaa hiyo, Nondo amemshukuru Mungu pamoja na mawakili wake waliosimama naye kuanzia mwanzo wa kesi hiyo, hadi leo alipoachiwa huru.

 

“Alhamdulilah, namshukuru Mungu sana, leo 23/12/2019, nimeshinda rufaa iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya maamuzi ya kesi niliyoshinda Novemba 5, 2018, nawashukuru mawakili wangu Jebra Kambole na Chance Luoga, Mtandao wa wWtetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), pia Mahakama, ndugu na watanzania” ameandika Abdul Nondo.

 

Nondo alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa taarifa za uongo kuwa alitekwa na watu wasiojulikana huku upande wa Jamhuri ukisema alijiteka mwenyewe.

 

Leave a Comment