
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi, leo Desemba 24, 2019 amemsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi wa Miliki nchini, Grayson Godfrey kwa kutosimamia ipasavyo taratibu za umiliki wa Nyumba za shirika za Nyumba HNC.
Akizungumza leo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Nyumba za shirika hilo zilizopo maeneo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Waziri Lukuvi amesema kuwa Mkurugenzi huyo hajitambui hivyo atafutwe mtu anayeweza kusimamia vyema kitengo hivho na ambaye anauweza kuendana na kasi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Aidha Waziri Lukuvi amesema kuwa kupanga kwa Nyumba hizo ni haki ya kila mtanzania huku akiwataka wale wote waliopangishwa majengo ya shirika kutoka kwa mtu binafsi tofauti na shirika hilo watoe taarifa kwake ili ampangishe moja bila kupitia kwa mtu binafsi.
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amewataka wahusika wanaojenga machinjio ya Vingunguti kutoka katika Shirika la Taifa NHC kutoa maelezo yankina ya kuhusu kutokamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.