
KILA ifikapo Desemba 25, ya kila mwaka, waumini wote wa dini ya Kikristo duniani husherehekea maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwokozi Yesu Kristo ambayo huitwa Sikukuu ya Krismas.
Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God, Dkt. Getrude Rwakatare ameendesha ibada ya Krismas kanisani kwake Mlima wa Moto, ambapo pia wamefanya sala maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Mgaufuli.