Rais Dkt. Samia Afunga Mkutano Mkuu Wa Maafisa Waandamizi Wa Jeshi La Polisi Kwa Mwaka 2024 – Video
Global Publishers September 14, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Picha mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania yanayoendelea Shule ya Polisi Tanzania-Moshi ambapo Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 17 Septemba, 2024 anafunga Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania, Viwanja vya Jeshi la Polisi CCP Mkoani Kilimanjaro, .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia akikagua gwaride la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Viwanja vya Shule ya Polisi Tanzania-Moshi leo Septemba 17, 2024.