
Polisi Mkoani Singida wanawashikilia Bashiri Hamisi, Hamisi Salumu na Hamida Hamisi wakazi wa Kijiji cha Irisya Wilayani Ikungi, Singida kwa tuhuma za kumuua mfanyabiashara wa ng’ombe Emmanuel Njovu na kumfunga kwenye mifuko miwili ya sandarusi kisha kuutumbukiza mwili wake chooni, RPC Singida amethibitisha.
Inadaiwa baada ya tukio hilo Hamisi alienda kwa Mganga wa kienyeji Manyara ili apewe dawa ya kuondoa mikosi na asikamatwe na Polisi, Mganga akamuambia ampeleke alipomfukia Marehemu.
Walipofika Mganga akaaga anaenda kutafuta dawa na akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa, Polisi wakafika na kumkamata mtuhumiwa, mwili umefukuliwa na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.