×

Mazishi ya Papa wa Zamani Benedict XVI Yatafanyika Jan 5, Kuongozwa na Papa Francis

Mazishi ya Benedict XVI yatafanyika Alhamisi Januari 5, 2023 na yataongozwa na Papa Francis, Vatican imesema.

Kiongozi wa Ujerumani atoa salamu za risala kwa mjerumani mwenzake

Benedict wa 16 ameelezewa kuwa mtu mwenye mzuri na Mjerumani mwenzake, Kansela Olaf Scholz.

Scholz alituma ujumbe wa Twitter akisema Papa huyo wa zamani alikuwa “kwa wengi, sio tu katika nchi hii, kiongozi maalum wa kanisa” Anasema mawazo yake yako kwa papa wa sasa, Francis.

Viongozi wa Ufaransa na Italia wasifia kazi ya papa wa zamani

Viongozi wa Ufaransa na Italia wametoa maoni yao kufuatia kifo cha papa huyo wa zamani.

Katika ujumbe wa Twitter, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatoa salamu za rambi rambi kwakumsofoa kiongozi huyo wa zamani wa Kanisa Katoliki kwa kuunda “ulimwengu wa kindugu zaidi”.

Alifanya hivyo kwa “nafsi na akili”, Macron anaongeza.Benedict XVI alikuwa “jitu la imani na akili”, anaongeza Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni katika ujumbe wake.

Anasema papa huyo wa zamani alizungumza na “mioyo na akili” za watu – na ataendelea kufanya hivyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza: Benedict alikuwa ‘mwanatheolojia mkubwa’

Salamu za rambi rambi kutoka kwa viongozi wa ulimwengu zinaendelea kutiririka kufuatia kifo cha papa wa Benedict XVI.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anasema amehuzunishwa na kifo cha Benedict XVI, ambaye anamtaja kama “mwanatheolojia mkuu”.

Sunak anaongeza ziara ya Benedict nchini Uingereza mwaka 2010 iliwakilisha “wakati wa kihistoria kwa Wakatoliki na wasio Wakatoliki kote nchini kwetu”.

Leave a Comment